By DW (Kiswahili) – January 6, 2017
Hiki ni kifaa kipya cha simu kinachokupa fursa ya kumrushia busu mwenzio aliye mbali na wewe kwa njia ya kidijitali, na akaweza kuhisi kama vile mnapokuwa karibu. Ili busu liweze kumfika unayemlenga, lazima naye awe na kifaa kama hiki. Kifaa cha ‘Kissenger‘ bado hakipatikani madukani lakini wewe unakionaje? Kweli busu la kidijitali linaweza kuwa sawa na la kweli?
(© Imagineering Institute)